Mkatoliki
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Ni moja, ni moja jana, ni moja leo
Ni moja asili yake ni Yesu Kristo
Ibada moja, sheria moja, mapokeo yale yale
Limeenea pande zote, ulimwengu mzima
(Najivunia) Nimezaliwa kwenye moja
Kanisa takatifu sana
Katoliki la mitume kweli
Nikabatizwa, mimi Mkatoliki *2
1. Liliwachwa mikononi mwa halifa wake, Mtume Petro
Alipokabidhiwa na Bwana Yesu alichunge Kanisa
Mridhi wake ndiye Papa wetu, Baba Mtakatifu
2. Sakramenti za kutuweka karibu kabisa na Mwenyezi
Ubatizo, ekaristi, kipaimara, upadre na ndoa
Na kitubio, mpako wa wagonjwa kujipatanisha na Baba
Simama eh tumshangilie Mungu, kwa zawadi ya imani Katoliki
a) Mkatoliki simama
b) Tusimame tulinde imani yetu
c) Sheria za kanisa ni nguzo yetu
d) Amri kumi za Mungu msingi wetu
e) Amri ya upendo yamaliza yote