Back to repertoire
Swahili

Yesu Ahsante Sana

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Yesu asante sana - Yesu asante sana *2
Kujifanya chakula - kujifanya chakula
Kujifanya chakula kutuletea shibe alama ya pendo *2
1. Wewe ndiwe chetu chakula cha uzima,
Kinatushibisha Yesu asante
2. Kila tunapokula mkate huu,
Tunapata uzima wa milele
3. Kila tunapokunywa kikombe hiki,
Tunapata uzima wa milele
4. Yesu aliwaosha wanafunzi wake,
Akawapa mfano wafanye vilevile
5. Alituamuru tufanye hivyo kwa ukumbusho,
Wa mwili na damu yake
6. Tunapofanya hivyo kwa moyo safi,
Twatangaza kifo cha Bwana wetu
7. Hapa duniani tunaishi kwa karamu,
Mbinguni tutaishi daima na Baba

Liturgical seasons

Mass parts

Thanksgiving