Back to repertoire
Swahili

Watumishi Wake Baba

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

1. Watumishi wake Baba wangapi waliopo;
Wanakula na kusaza chakula chake Baba
Nami nataabika hapa; Nashiriki na nguruwe
Chakula kisichofaa, yanipasa kurudi
Nitarudi na kusema; Baba yangu nisamehe
Nimekosa kwake Mungu, na mbele yako Baba
2. Baba kamwona yu mbali kashikwa na huruma;
Akakimbia kumlaki kamkumbata na busu.
3. Baba sistahili tena kuitwa mwana wako;
Unifanye kama mmoja wa watumishi wako.
4. Baba yangu nimekosa ninaomba huruma;
Unisamehe nirudi nikakutumikie.
5. Nasongea ninakuja ninakukimbilia;
Mimi ni mtoto mpotevu Baba unipokee.

Liturgical seasons

Mass parts

Offertory
Communion
Watumishi Wake Baba — Community Choir