Back to repertoire
Swahili
Utukuzwe Ewe Baba Mungu Utukuzwe
Also known as: Utukuzwe Ewe Baba · Utukuzwe Ewe Baba Mungu
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Utukuzwe ewe Baba Mungu utukuzwe - Aleluya
Kwani Yesu mfufuka ametualika – Aleluya
Utukuzwe – Utukuzwe, Baba muumba ulimwengu – aleluya *2
2. Tumepokea mkate, mazao ya mashamba -
Ndiyo alama kwetu, ya wema wako mkuu—
3. Ni tunda la bidii, ya mkono na ya moyo—
Jalie iwe kwetu, chakula cha uzima—
4. Zawadi ya divai, kutoka mizabibu—
Ndiyo alama kwetu, ya wema wako mkuu—
5. Ni tunda la bidii, ya mkono na ya moyo—
Jalie iwe kwetu, kinywaji cha kiroho—
6. Sifa kwako ee Mungu, kwa kuotesha mkate—
Shukrani kwako Baba, kwa kutulisha sisi—
7. Utukuzwe, Ee Mungu, uliyetuchagua -
Tuwe taifa lako na kukutumikia
Liturgical seasons
Mass parts
Offertory