Back to repertoire
Swahili

Usia wa Maria

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Sisi wana dunia tukumbuke maneno, aliyosema Bikira Maria
Alipowatokea watoto wa Fatima, Lucia Francisi na Yasinta

Alisema tusali, tusali rosari, tupate amani
Na tuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi
Na wasiomwamini Yesu Mwokozi wamuamini ili waokoke

1. Mama yetu anahuzunishwa sana, kwa matendo yetu maovu
Anajua adhabu yetu ijayo, hivyo anaona huruma sana
2. Atusihi tuache dhambi kwa dhati, tuache kumkosea Yesu
Tuyatubu makosa yetu yote, ili Bwana atupatie amani
3. Tusitende maovu na dhambi, atusihi mama wa Yesu,
Tusimkasirishe tena Mungu, asije tutupa motoni milele
4. Ibada ya moyo safi wa Maria, tuizingatie daima.
Tuipokee komunyo Takatifu kila juma mosi ya kwanza ya mwezi.

.

Liturgical seasons

Mass parts