Back to repertoire
Swahili

Uje, Roho Mtakatifu

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu
Roho zetu kwa mwangao
Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji
Uje mwanga wa mioyo
Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwa(a)nana
Ewe raha mustarehe
Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto, burudisho
U mfutaji wa machozi
Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini
Neema yako mioyoni
Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu
Kwake yote yana kosa
Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu
Na kuponya majeraha
Ulegeze ukaidi, pasha moto ubaridi
Nyosha upotevu wote
Wape waamini wako, wenye tumaini kwako
Paji zako zote saba
Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila ila,
Wape heri ya milele
Amina aleluya, amina, aleluya,
Amina, aleluya

Liturgical seasons

Mass parts

Entrance
Uje, Roho Mtakatifu — Community Choir