Back to repertoire
Swahili

Niseme Nini Basi

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Niseme nini basi juu ya Mama yetu Maria (Mama Bikira Maria)
Mama mpendelevu Mama mwenye neema
1. Wakati wa majaribu mwombezi wetu ni Maria (mama yetu)
Wakati wa mashaka kimbilio letu ni Mama (Maria)
2. Mama uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili (mama yetu)
Ukamzaa mwana mkombozi wa ulimwengu (Maria)
3. Moyo wako wa heri, moyo safi, moyo mweupe (mama yetu)
Nijalie neema nishinde majaribu yote (Maria)
4. Mama wa mkombozi mnara wetu wa Mbinguni (mama yetu)
Mwangaza wetu sisi tunaosafiri gizani (Maria)
5. Shika mkono wangu nionyeshe njia ya kweli (mama yetu)
Nifike kwa mwanao anapoketi uwinguni (Maria)

Liturgical seasons

Mass parts