Back to repertoire
Swahili
Ninataka Kuingia Mjini Mwa Mungu
Also known as: Ninataka Kuingia Mjini
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Ninataka kuingia, mjini mwa Mungu
Nitashinda nitakaza mwendo nifike
Nikiishi kwa shida, ni kichoka njiani
Yesu unaniambia ‘Uningojee’
2. Naitwa na Yesu Kristu enzini mwake
Nimkimbilie Bwana kamwe sisiti
Wote wachelewao hawatapa ’TAJI’
Mimi sitaki kingine ila ‘Uzima’
3. Elekeza macho yangu Mlangoni Pako
Niongoze nipe nguvu nikilemewa
Ninapojaribiwa, ninaposingiziwa
Yesu unisaidie nisikuache
4. Unishike mkono Bwana nisianguke
Najiona kuwa mnyonge ‘Nguvu’ ikwako
Neno lako ‘Taa Yangu’ linanipa uzima
Nikifika nitaimba ‘Umeniponya’
Liturgical seasons
Mass parts
Entrance