Back to repertoire
Swahili

Nimeahidi Yesu

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

1. Nimeahidi Yesu - kukutumikia
Wewe u Bwana wangu - u rafiki pia
Sitaogopa vita - wewe ndiwe mweza
Sitaiacha njia – ukiniongoza
Imbeni aleluya, aleluya, imbeni
Shangwe kwa Bwana Yesu, ndiye mweza wetu
2. Dunia i karibu -Bwana siniache
Na mengi majaribu -yako pande zote
Siku zote adui - ni ndani na nje
Bwana Yesu nivute - karibu na wewe
3. Nikusikie wewe Bwana - nenda nami Bwana
Kelele za dunia - ndizo nyingi sana
Nena kunihimiza - au kunionya
Nena nikusikie - mwenye kuniponya
4. Umewapa ahadi – wakufuatao
Kwenda uliko wewe - wawe huko nawe
Nami nimeahidi - kukutumikia
Nipe neema Bwana - ya kukuandama
5. Hatua yako Bwana - na nizikanyage
Wewe u mwenye nguvu - mimi ni mnyonge
Niongoze nivute - nishike daima
Mwishoni niwasili - mbinguni salama

Liturgical seasons

Mass parts

Recessional
Nimeahidi Yesu — Community Choir