Nikupe Nini Mungu Wangu
Also known as: Nikupe Nini
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Offertory
Nikupe nini Mungu wangu, nikupe nini we Mwokozi,
nikupe nini Bwana Wangu chakukupendeza.
1. Nakutolea mkate toka mmea wa ngano, nakutolea divai ni tunda la mzabibu
Ninakuomba Mwokozi, nifanyie msamaha na unipokee.
Mema unayoyatenda, nitafanya nini mimi nikurudishie.
2. Kila nitakachoshika mbona bado ni kidogo, mema unayoyatenda kwangu mimi naogopa
3. Mchana hata usiku wewe wanisimamia na nikiwa safarini waniepusha ajali
4. Nikiwa na matatizo Bwana wanisimamia, nikiwa kwenye majonzi wewe unanifariji
5. Kama njia sioni wewe unaniongoza, na hata nikopotea kwako unanirudisha
Nitafanya nini mimi kitakachokuwa sawa na fadhili zako,
nitaimba vipi mimi niyataje mema yote utendayo kwangu
Offertory
Nikupe nini Mungu wangu
Nikupe nini Mungu wangu cha kukupendeza
Cha kukupendeza, cha kukupendeza Cha kukupendeza,
Cha kupendeza, siku hii ya leo
1. Ninacho kidogo, cha kukupendeza, ewe Mungu wangu
Ninachoandaa siku hii ya leo ndicho hiki Bwana
2. Sadaka ya leo, ni sadaka safi, isiyo na doa
Twakuomba Bwana twakuomba Bwana upendezwe nayo