Back to repertoire
Swahili
Ni Nyota
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Mama yetu Maria, ni mama wa neema,
tena ni kimbilio la watu wote wakosefu,
ni msaada wa kweli mama tuombee.
Ni nyota (*n) Mama yetu Maria
Ni nyota ya matumaini
2. Mlango wa mbinguni, sanduku la agano,
malkia wa amani, malkia mwenye huruma,
Mama mpendelevu mama tuombee
3. Nyota ya asubuhi, ni mnara wa pembe
Kimbilio la wakosefu mama utuombee
Mama yetu Maria kiongozi wetu
4. Twakushukuru mama kwa maombezi yako
Na kwa neema zote unazo tuombea mama
Malkia wa amani Mama tuombee
.