Back to repertoire
Swahili
Nawapa Amri
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Nawapa amri! Amri pendaneni,
Asema Bwana; Kama vile mimi nilivyowapenda nyinyi
(Nanyi) Nanyi pia pendaneni (Tupendane)
1. Wapenzi na tupendane, Neno latoka kwa Mungu,
Na pia apendaye amezaliwa na Mungu,
[Naye] Naye anamjua Mungu (Tupendane)
2. Yule asiye na pendo, hakumjua Mungu wetu
Kwa maana Mungu ni mwenye upendo kamili
[Naye] Naye ametuamuru (Tupendane)
3. Mungu apenda dunia, kwa mapendo yake kwetu
Akamtuma mwanaye mwana wake wa pekee
[Hapa] Hapa kwetu duniani (Tupendane)
4. Kila amkiriye Yesu, kuwa ni mwana wa Mungu
Ndipo Mungu akaa ndani yake mtu yule
[Naye] Naye ndani yake Mungu (Tupendane)