Naondoka Mimi
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Naondoka mimi naenda kwa Baba nipeleke hiki nilichokipata,
japo kidogo, sitaona haya, nimeamua sitarudi nyuma
Nakuja pole pole (Baba) nakuja na zawadi (yangu)
naleta mbele zako (ili) nitoe shukrani *2
2. Natembea mimi mwendo wa madaha nakanyanga chini kwa maringo tele,
naelekea altari ya Bwana, nimkabidhi nilichojaliwa
3. Nimechangamka ninashangilia napiga kelele, kelele za shangwe,
nacheza cheza najongea kwako, ee Mungu wangu nipokee mimi
4. Nafsi yangu mimi naileta kwako, mkate divai mimi ninaleta,
Uvigeuze mwili na damuyo, chakula chetu tunaosafiri
5. Mavuno shambani mimi nimevuna, mifukoni fedha nimefanikiwa,
mimi ni nani nisikushukuru, Baba nasema ahsante kwa yote.