Back to repertoire
Swahili
Nalifurahi Waliponiambia
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Nalifurahi waliponiambia twende nyumbani mwa Bwana *4
Wololololo!
Twende nyumbani twende (twende) nyumbani
Njooni (twende) tuingie nyumbani mwake Bwana Mungu.
Inapendeza!
Twende nyumbani twende (twende) nyumbani
Njooni (twende) tuingie nyumbani mwake Bwana Mungu.
2. Nyumba ya Mungu ya kuabudiwa njooni tukamuabudu. *2
Nyumba ya Mungu inayopendeza kweli imejaa Baraka. *2
3. Nyumba ya Mungu ni yenye amani pia ni yenye upendo *2
Tufurahie nyumbani ya Mungu kwani ni yenye furaha *2
4. Tucheze ngoma kinanda kinubi, gita kayamba na zeze *2
Tumuimbie anayestahili kwani ni Mungu milele. *2
Liturgical seasons
Mass parts
Entrance