Back to repertoire
Swahili
Nainua Moyo Wangu
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Nainua moyo wangu kwako wewe, ee Baba;
Unikinge na uovu, tumaini wewe tu.
2. Nijulishe njia zako, nifundishe ukweli;
Hekimayo niongoze, tumaini wewe tu
3. Ewe Baba, ukumbuke wema wako milele
‘nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu.
4. Nitazame kwa huruma, ewe Mungu amini;
‘nitubishe, mwenye dhambi, tumaini wewe tu
5. Shida zangu angalia, ‘niokoe dhikini;
‘nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu.
6. Njia zako zote Bwana, ni fadhili na kweli;
‘niongoze, mtoto wako tumaini wewe tu.
Liturgical seasons
Mass parts
Entrance