Back to repertoire
Swahili
Mwili wa Bwana Yesu
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Mwili wa Bwana Yesu, chakula cha Mbingu
Ni chakula cha roho, chenye uzima
Hima uwe nasi ee Bwana Yesu
Ukatushibishe chakula bora
Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
2. Yesu alituambia, Yeye ni chakula
Ni chakula cha roho, chenye uzima
Sote twaamini, ni mwili wake
Pia twaamini ni damu yake
Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
3. Yesu alituambia, kuwa tumpokee
Ni chakula cha roho, chenye uzima
Ee Bwana mkombozi tunakuomba
Kwa chakula hiki tuimarike,
Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
4. Hii ndiyo karamu, alituachia
Ni chakula cha roho, chenye uzima
Aulaye mwili na kunywa damu
Anao uzima wa siku zote
Ni chakula cha roho, chenye uzima *2
Liturgical seasons
Mass parts
Communion