Back to repertoire
Swahili

Mshukuruni Mwokozi

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Mshukuruni mwokozi enyi mataifa,
pigeni vigelegele pigeni makofi *2
Tangazeni rehema zake leo asubuhi,
semeni ya kuwa Bwana ni mwenye adili *2

1. Njooni tumwimbie Bwana, Baba wa Mwokozi wetu,
mikononi mwake zimo pande za dunia,
bahari ni yake ndiye alieumba, na mikono yake ilituumba sisi.
2. Bwana ametamalaki mataifa yatasema, ameketi juu ya
makerubini mbinguni, yeye Bwana katika sayuni ni
mkuu, kazunguka juu ya mataifa yote.
3. Mshangilieni Bwana mwimbieni na zaburi
vinanda na baragumu vyote mpigieni.
mshukuruni bwana kwa kuwa ni mwema
kwa kuwa fadhili zake ni za milele.

Liturgical seasons

Mass parts

Thanksgiving