Back to repertoire
Swahili

Moyo Wangu Wamtukuza Bwana

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

(Moyo) Moyo wangu wamtukuza Bwana
(Roho) Roho yangu inafurahi *2
1. Kwa kuwa amemwangalia, kwa huruma mtumishi wake,
Hivyo tangu sasa watu wote, wataniita mwenye heri.
2. Kwa sababu Mwenyezi Mungu, amenitendea makuu,
(Jina lake ni takatifu) *2
3. Huruma yake ni kwa wote, wote wale wanaomcha,
(Vizazi hata na vizazi) *2
4. Huyatenda mambo makuu, kwa nguvu za mikono yake,
(Wenye kiburi hutawanya) *2
5. Hushusha wote wenye vyeo, kutoka vitini vya enzi,
Nao wote wanyenyekevu, wote hao huwainua
6. Huwashibisha wenye njaa, na matajiri huwaacha,
(Waende mikono mitupu) *2
7. Huilinda taifa lake, teule la mtumishi wake,
(Hukumbuka huruma yake) *2
8. Kama alivyowahidia, babu zetu kuwasaidia,
(Ibrahimu na uzao wake) *2
9. Atukuzwe Baba na Mwana, naye Roho Mtakatifu
Leo kesho hata milele, kwa shangwe milele Amina.

Liturgical seasons

Mass parts