Back to repertoire
Swahili

Misa Taita

Also known as: Sanctus – Misa Taita

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Gloria

V. Tukufu! W. Tukufu kwa Mungu juu
V. Amani! W. Na amani duniani
V. Kwa watu wenye mapenzi W. Wenye mapenzi mema *2
V. Sifa! W. Sisi tunakusifu
V. Heshima! W. Sisi tunakuheshimu
V. Tunakuabudu! W. Sisi tunakuabudu *2
V. Tukufu! W. Sisi tunakutukuza
V. Shukrani! W. Sisi tunakushukuru
V. Kwa ‘jili ya utukufu! W. Utukufu wako mkuu *2
V. Ee Mungu! W. Ee Bwana Mungu
V. Ee Baba! W. Mfalme wa mbinguni
V. Ee Mungu Baba W. Mungu Baba Mwenyezi *2
V. Ee Bwana! W. Eh Bwana Yesu Kristu
V. Eh Mwana! W. Kristu Mwana wa pekee
V. Mwana wa Baba W. Mwana Kondoo wa Mungu *2
V. Mwokozi! W. Mwenye kuondoa dhambi
V. Huruma! W. Dhambi za dunia
V. Utuhurumie! W. Pokea ombi letu *2
V. Ee Yesu! W. Kwani ndiwe Mtakatifu
V. Ee Kristu! W. Kwani ndiwe Bwana
V. Ee Yesu Kristu! W. Ndiwe peke yako Mkuu *2
V. Umoja! W. Pamoja na Roho Mtakatifu
V. Milele! W. Katika utukufu
V. Tukufu wa Mungu Baba W. Kristu anaishi *3

Sanctus

V. Mtakatifu Bwana Mungu wetu W. Ee, Hosana juu!
V. Mtakatifu Bwana Mungu wetu W. Ee, Hosana juu!
V. Mtakatifu Bwana Mungu wetu W. Ee, Hosana juu!
W. Mbinguni.
1. Utukuzwe Bwana Mungu W. Ee!
V. Mungu Muumba wetu W. Ee!
V. Mbingu na dunia zimejaa Utukufu wako W. Ee! Ee! Ee! Ee, hosanna juu
V. Ee, Ee, mbinguni W. Mbinguni
2. Utukuzwe Bwana Mungu W. Ee!
V. Mungu Mkombozi wetu W. Ee!
V. Uliangamiza mauti ukaleta uzima mpya W. Ee! Ee! Ee! Ee, hosanna juu
V. Ee, Ee, mbinguni W. Mbinguni
3. Utukuzwe Bwana Mungu W. Ee!
V. Mungu Mfariji wetu W. Ee!
V. Ulimtuma Roho kwetu tuwe sote mwili mmoja W. Ee! Ee! Ee! hosanna juu, mbinguni
V. Ee, Ee, mbinguni
V. Mtakatifu....

Mystery Of Faith

V. Kristu, Kristu, Ee! W. Kristu alikufa
V. Kristu, Kristu, Ee! W. Kristu alifufuka
V. Kristu, Ee Kristu, Kristu! W. Atakuja tena, Kristu

Liturgical seasons

Mass parts

Gloria
Sanctus
Mystery of Faith
Agnus Dei
Offertory
Misa Taita — Community Choir