Misa Shukrani
Also known as: Sanctus – Misa Shukrani
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Gloria
Utukufu kwa Mungu mbinguni, na amani duniani kote,
{Kwao wenye mapenzi mema} *2
1. Tunakusifu, tunakuheshimu, twakuabudu, nakukutukuza.
2. Twakushukuru, mwenye utukufu, Mfalme wa mbingu, Mungu Baba yetu.
3. Ee Bwana Yesu, Mwana wa pekee, Mwana kondoo wake Mungu Baba.
4. Mwenye kufuta dhambi za dunia, ‘tuhurumie, utusikilize.
5. Unayeketi kuume kwa Baba, u peke yako, Mkuu, Yesu Kristu.
6. Pamoja nawe Roho Mtakatifu kwa utukufu wake Mungu Baba.
Sanctus
Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ewe Bwana,
{Bwana wetu Mungu wa majeshi} *2
1. Mbingu na dunia zimejaa utukufu, kweli zimejaa wako utukufu;
{Hosanna! Hosanna! Hossana! Hossana juu mbinguni} *2
2. Amebarikiwa yule mwenye kuja kwetu - yule mwenye kuja, kwa jina la Bwana
{Hosanna! Hosanna! Hossana! Hossana juu mbinguni} *2
Kyrie
Tunakuomba ewe Bwana, utuhurumie, sisi wakosefu, utuhurumie x2
Tunakuomba ewe Kristu, utuhurumie, dhambi tunatubu, utuhurumie x2
Tunakuomba ewe Bwana, utuhurumie, sisi wakosefu, utuhurumie x2
Mystery Of Faith
Yesu Kristu alikufa, Yesu Kristu alifufuka,
{Yesu Kristu atakuja tena} *2