Misa Mt. Paulo
Also known as: Misa Paulo · Sanctus – Misa Paulo
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Gloria
R. Utukufu, utukufu, utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani duniani kwa watu Wenye mapenzi mema
1. Tunakusifu Bwana, tunakuheshimu,
Tunakuabudu, tunakutukuza,
{Tunakushukuru} *2
{Kwa ajili ya utukufu wako mkuu} *2
2. E e Bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni,
E e Bwana Mungu, Mungu Baba Mwenyezi.
E Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee.
E Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee.
Ee Bwana Mungu, {Mwana kondoo wa Mungu, Mwana wa Baba} *2
3. Mwenye kuondoa dhambi za dunia,
Utuhurumie, Pokea ombi letu.
{Ewe mwenye kuketi} *2
{Kuume kwa Baba, utuhurumie} *2
4. Kwa kuwa ndiwe: peke yako Mtakatifu,
Peke yako Bwana, Mkuu; Peke yako Yesu Kristu.
Pamoja na Roho, Roho mtakatifu,
{Katika utukufu wa Mungu Baba} *4
Kyrie
1. Wewe uliyetumwa kuwaponya wanaojuta dhambi
Ee Bwana utuhurumie, Ee Bwana utuhurumie,
Bwana, Bwana, ee Bwana, Ee Bwana utuhurumie.
2. Wewe uliyekuja kuwaita wakosefu
Ee Kristu, utuhurumie, Ee Kristu, utuhurumie
Kristu, Kristu, ee Kristu, Ee Kristu, utuhurumie
3. Wewe unayeketi kuume kwa Baba, ukituombea,
Ee Bwana utuhurumie, Ee Bwana utuhurumie,
Bwana, Bwana, ee Bwana, Ee Bwana utuhurumie.
Sanctus
Mtakatifu *3 Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia! Zimejaa, Utukufu wako Bwana.
Hosana juu *3 Mbinguni.
Mbarikiwa anayekuja; kwa jina la Bwana.
Hosana juu *3 Mbinguni
Mystery Of Faith
Kristu alikufa *2, Kristu alifufuka
Kristu atakuja tena.
Gospel Acclamation
Alleluiyah *n
Gospel Acclamation
Alleluia *n
Great Amen
Amen! *n
Great Amen
Amina *n