Misa Mchanganyiko
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Gloria
Utukufu juu mbinguni kwa Mungu,
Na amani duniani kwa watu.
1. Tunakusifu, tunakuheshimu, twakuabudu na kukutukuza.
2. Twakushukuru, mwenye utukufu, mfalme wa mbingu, Mungu Baba yetu.
3. Ee Bwana Yesu, Mwana wa pekee, uliye Mwana kondoo wa Mungu.
4. Mwenye kufuta dhambi za dunia, ‘tuhurumie, utusikilize.
5. Unayeketi kuume kwa Baba, u peke yako Mkuu, Yesu Kristu.
6. Pamoja naye Roho Mtakatifu katika utukufu wake Baba.
Sanctus
Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako
Hosana juu, Hosana, hosana juu mbinguni
Mbarikiwa mwenye kuja kwa jina la Bwana.
Hosana juu, Hosana, Hosana juu mbinguni
Kyrie
Ewe Bwana, Bwana, Bwana Ewe Bwana *2
Ewe Bwana, utuhurumie *4
Ewe Kristu, Kristu Kristu ...
Ewe Bwana, Bwana, Bwana...