Back to repertoire
Swahili

Misa Kariobangi

Also known as: Sanctus – Misa Kariobangi

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Gloria

Utukufu juu kwa Mungu, Utukufu juu mbinguni
Na amani kote duniani, Kwa wenye mapenzi mema

1. Tunakusifu, tunakuheshimu; twakuabudu, tunakutukuza
Twakushukuru kwa ajili, ya Utukufu wako mkuu
2. Ewe Mungu, ndiwe Mfalme; wa mbinguni, Baba Mwenyezi,
Ewe Bwana Yesu Kristu, wa pekee Mwana wa Baba
3. Ewe Yesu Mwanakondoo, wa Mungu Mwana wa Baba
Ewe Mwenye kuziondoa Dhambi zetu ‘tuhurumie
4. Ewe Mwenye kuziondoa; za dunia dhambi za watu
Ewe mwenye rehema nyingi Upokee maombi yetu
5. Uketiye kuume kwake; Mungu Baba ‘tuhurumie
Kwa kuwa ndiye uliye Peke yako Mtakatifu
6. Peke yako ni Wewe Bwana; peke yako Bwana Mungu
Peke yako ni Mkombozi Peke yako Yesu Kristu
7. Naye Roho Mtakatifu, katika ‘tukufu wake
Mungu Mmoja anayeishi Na kutawala milele yote

Sanctus

Viongozi: (Bass) Mtakatifu Wote: Mtakatifu mtakatifu Bwana Mungu
V. (Bass) Wa majeshi W. Mbingu na dunia zimejaa ‘tukufu wako
V. (Tenor) Hosanna! W. Hosana juu Mbinguni x2
V. (Tenor) Hosanna! W. Hosana juu Mbinguni
V. (Bass) Mbarikiwa W. Anayekuja kwa jina lake Bwana Mungu x2
V. (Tenor) Hosanna ...

Agnus Dei

V. (Soprano) Ee Mwana Kondoo
W. Uondoaye dhambi za dunia, utuhurumie *2
V. (Tenor) Ee Mwana Kondoo
W. Uondoaye dhambi za dunia, utujalie amani

Mystery Of Faith

V. Kristu W. Alikufa
V. Kristu W. Alifufuka
V. Kristu Yesu W. Alikufa, Alifufuka, Atakuja tena

Liturgical seasons

Mass parts

Gloria
Sanctus
Mystery of Faith
Agnus Dei
Offertory