Back to repertoire
Swahili

Misa Akamba

Also known as: Kamba Mass · Akamba Mass

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Gloria

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwao watu wa mapenzi,
wenye mapenzi mema.
Tunakusifu (Baba) tunakuheshimu, tunakuabudu (Baba) tunakutukuza
2. Baba tunakushukuru kwa ajili ya utukufu, utukufu wako mkuu.
3. Ewe Mungu ni Mfalme wa mbinguni Mungu Baba, Baba ndiwe Mwenyezi.
4. Ewe Bwana Yesu Kristu ndiwe Mwana wake Mungu ndiwe Mwana wa pekee.
5. Ewe Bwana Mungu Mwana koondoo wake Mungu, Mwana wake Baba.
6. Ewe mwenye kuondoa zetu dhambi za dunia Bwana utuhurumie.
7. Ewe mwenye kuondoa zetu dhambi za dunia, ombi letu pokea.
8. Ewe mwenye kuketi kuume kwake Baba, ewe utuhurumie.
9. Ni kwa kuwa ndiwe uliye peke yako mtakatifu, Bwana Yesu Kristu.
10. Na pamoja naye Roho mtakatifu katika utukufu wa Mungu Baba.

Sanctus

{Mtakatifu Bwana *3 Mungu wa majeshi} x2
1. Mbingu na dunia zimejaa utukufu utukufu wako;
Hosana juu mbinguni, Hosana! Hosana! Hosana ee juu mbinguni *2
2. Mbarikiwa ajaye kwa jina lake Bwana,
Hosana juu mbinguni, Hosana! Hosana! Hosana ee juu mbinguni *2
Mtakatifu Bwana, Mungu wa majeshi *2
.

Mystery Of Faith

Yesu Kristu alikufa, Yesu Kristu alifufuka,
{Yesu ee Yesu Kristu atakuja tena} *2

Great Amen

Amina *n

Liturgical seasons

Mass parts

Gloria
Sanctus
Mystery of Faith
Amen
Agnus Dei