Back to repertoire
Swahili

Mimina

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

1. Mimina, kama vile zilivyojaa juu,
Mimina ziteremshe tuzipokee, Bwana
Mimina neema zako, mimina, kati yetu,
Mimina neema tele, mimina, Mungu wetu,
Mimina leo neema nyingi mimina, tufurahi
Mimina, Bwana mimina,
leo mimina ee Bwana mimina.
Mimina neema zako, mimina, kati yetu,
Mimina neema tele, mimina, Mungu wetu,
Mimina leo neema nyingi mimina, tufurahi
Mimina, Bwana mimina,
leo mimina neema mimina
2. Mimina, ulivyomimina kwa Abrahamu,
Mimina, uwamiminiavyo wamchao, Bwana
3. Mimina, tujae nguvu za kukutukuza,
Mimina, tukazieneze sifa zako, Bwana
Twakuinulia mikono, huko uliko juu,
Tazama wana wako, tunaomba neema)
Mimina neema mimina (Bwana Mungu),
Mimina neema mimina,
Tunaomba Bwana (ewe Mungu) mimina,
mimina neema mimina;
Mimina kwa wote tulioko hapa tujaze neema mimina,
Mimina hata kwa walioko mbali
peleka neema mimina,
1. Mimina usiku mimina mchana (hee!)
mimina neema mimina,
2. Mimina masika mpaka kiangazi (hee!)
daima neema mimina,
Mimina neema mimina (Bwana Mungu),
mimina neema mimina daima!

Liturgical seasons

Mass parts

Thanksgiving
Mimina — Community Choir