Back to repertoire
Swahili
Mfalme wa Amani
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Mfalme wa amani mpeni heshima,
Yerusalem mjini anaingia
Na unyenyekeo na upole mkuu,
Anapanda punda Mwana wa Mungu.
Hosana juu, hosana Juu, hosana juu.
2. Njooni Mahebruni, njooni watoto,
Leteni matawi ya kumsalimu.
Mwana wa Daudi kweli Masiya
Anakuja kwenu mwenye huruma.
3. Tandikeni nguo miguuni pake,
Imbeni zaburi, shangilieni.
Mbarikiwa huyu ajaye kwetu
Kwa Jina la Bwana Mkombozi mkuu.
4. Ufurahi sana, we` Yerusalem
Yule wamwabudu roho za mbingu.
Na huruma pale anakujia,
Haki na amani akuletea.
5. Ndimi za wachanga zafumbulia,
Kwa mwujiza sifa yake Masiya
Na makundi yote ya malaika
Sifa na heshima wanamtolea.
Liturgical seasons
Mass parts
Recessional