Mama Pale Msalabani (Stabat Mater)
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Mama pale msalabani macho yatoka machozi
Akimwona Mwanaye, akimwona mwanaye.
2. Kweli vile akilia, uchungu kama upanga
ukampenya moyowe, ukampenya moyowe.
3. Mwenye moyo mgumu, nani? Asimhurumie basi, mama mlilia
Mwana? Mama mlilia mwana?
4. Ewe mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
moyo wangu m’nye dhambi, Moyo wangu m’nye dhambi.
5. Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie, pamoja na
Ukombozi, pamoja na ukombozi.
6. Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi wa uchungu na
msiba, wa uchungu na msiba.
7. Nisianguke motoni uniweie Msimamizi, Ewe Bikira mwema,
Ewe Bikira mwema.
8. Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho, Ewe Mwokozi
wangu, Ewe Mwokozi wangu.
9. Nitakapokufa mimi upokee roho basi,
niende kwako Mungu, niende kwako Mungu.