Back to repertoire
Swahili
Leteni Sadaka Kamili
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Leteni sadaka kamili ghalani *2
{Ili chakula kiwemo katika nyumba yangu,
Asema Bwana, Bwana wa majeshi} *2
1. Mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana
Nitafungua milango ya mbingu, asema Bwana
Na kuwamwagia baraka tele, asema Bwana
2. Mimi ndimi mgawa wa vipaji, asema bwana
Nitawaongezea maarifa, asema Bwana
Ya kuyashinda magumu yoyote, asema Bwana
3. Mtakachokiomba nitawapa, asema bwana
Nitawapa vyeo na mali nyingi, asema Bwana
Nakuuondoa umasikini, asema Bwana
4. Nitawalinda na kuwasitawisha, asema Bwana
Nanyi mtazaa matunda bora, asema Bwana
Yatakayo dumu milele yote, asema Bwana
Liturgical seasons
Mass parts
Offertory