Back to repertoire
Swahili
Inakuaje Tunasikia Maneno
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Inakuwaje tunasikia maneno, wanayosema,
kwa lugha yetu wenyewe
Tunasikia mambo hayo ya Mungu, wanayosema,
kwa lugha yetu wenyewe
{Wao ni wa Galilaya, na si ni wa makabila,
Ya kutoka nchi mbalimbali (duniani)
Ina maana gani, linashangaza jambo hilo } *2
1. Siku ile ya Pentekoste ilipofika,
mitume nao waamini
Walikusanyika pamoja katika nyumba,
walimokuwa wamekaa
2. Mara uvumi wa upepo ukasikika,
ndimi za moto zikawashukia,
Wakawa wamejazwa na Roho Mtakatifu,
wakisema lugha nyingi