Back to repertoire
Swahili
Hodi Hodi Nyumbani
Also known as: Hodi Hodi
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Hodi hodi nyumbani mwako Bwana, ninabisha nifungulie
Nimekuja nyumbani mwako leo, nimekuja kukuabudu,
Kwa unyenyekevu naijongea, meza yako yenye baraka
Nakuja na sala zangu Ee Bwana, nakuomba zisikilize
Ninakutolea sadaka safi, Mungu Baba uipokee.
1. Nyua za Bwana zapendeza, zinapendeza macho kama nini
Natamani kuingia hekaluni, nikamwabudu
2. Nimeingia hekaluni, nimeingia hekaluni mwako
Nimekuja kuabudu kusujudu, nyumbani mwako
3. Unipokee Mungu wangu unitakase, mimi mwenye dhambi
Nimekuja mbele zako Mungu Baba, unipokee
Liturgical seasons
Mass parts
Entrance