Back to repertoire
Swahili

Heri Hao

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

Heri hao walio kamili, Wafuatao sheria za Bwana,
na kutenda yaliyo ya haki.
Heri wenye kumtii Jehova, Na kwa moyo watamtafuta,
na kufuata hizo njia zake.

Naam hawakutenda ubatili, wamezifuata hizo njia zake.
Wewe umetupa mawaidha yako, ili sisi tuyatii yote.
Ningependa, njia zangu ziwe ni thabiti.
Ningependa, Mungu nifuate amri zako,
Ndipo mimi sitaaibika nikifuata maagizo yako.

Ntakusifu kwa moyo wa unyofu (Bwana!)
Nikiisha jifunza hukumu (niitatii)
Nitatii amri, usiniache. *2

Jinsi gani mimi nisafishe njia yangu?
Ni kwa kutii na kufuata njia yako.
Moyo wangu umekutafuta Bwana.
Usiniache nipote mbali; niyaache maagizo yako (moyoni)

Moyo wangu waweka neno lako,
Ee Bwana, kutenda dhambi sitaki.
Neno la Bwana litasimama imara huko mbinguni moyoni.
Moyo wangu naweka neno lako,
Ee Bwana. Ee Bwana, ninakupa moyo wangu.
Uniokoe niwe wako milele.
Nisife na dhambi; Ee Bwana ninakupa moyo wangu, unipokee!

Liturgical seasons

Mass parts

Offertory
Communion
Thanksgiving
Recessional
Heri Hao — Community Choir