Centenary Mass
Also known as: Misa Centenary · Centenary · Sanctus – Centenary Mass · Misa Centinary
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Gloria
1. Utukufu kwa Mungu juu Mbinguni, Na amani iwe
kwa watu wenye mapenzi mema duniani kote.
(Tunakusifu) tunakusifu, tunakeheshimu, tunakuabudu, tunakutukuza *2
2. Tunakushukuru Mungu kwa ajili, Ya utukufu wako mkuu ee Bwana,
ni Mungu ndiwe mfalme wa mbinguni
3. Ee Baba Mwenyezi Bwana Yesu Kristu, Ee Mwana wa pekee
ee Mungu Mwanakondoo wa Mungu Mwana wake Baba.
4. Mwenye kuondoa dhambi za dunia, Utuhurumie,
tuhurumie maombi yetu Bwana uyapokee.
5. Mwenye kuketi kuume kwa Baba, Utuhurumie kwa kuwa ndiwe
pekee yako ni mtakatifu.
6. Pekee yako Bwana pekee yako mkuu, Ewe Yesu Kristu pamoja naye
Roho Mtakatifu milele yote
Our Father
Baba Yetu wa Mbinguni Baba! Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako ufike Baba Utakalo lifanyike
1. Duniani kama mbinguni Baba - utakalo lifanyike
Tupe leo mkate wetu Baba -
Mkate wetu wa kila siku Baba -
2. Tusamehe makosa yetu,
Kama vile tunavyowasamehe
Waliotukosea sisi, Utakalo lifanyike.
3. Situtie kishawishini Baba –
Walakini utuopoe Baba -
Maovuni utuopoe Baba –
4. Kwa kuwa ‘falme ni wako Baba -
Na nguvu na utukufu Baba -
Utukufu hata milele Baba –
Sanctus
V: Mtakatifu, mtakatifu, W: Mtakatifu, Bwana Mungu.
V: Mtakatifu, mtakatifu, W: Mtakatifu Bwana Mungu, wa majeshi *2
Mbingu na dunia zimejaa utukufu
{Mbingu na dunia} *3 Zimejaa utukufu wako,
Zimejaa utukufu wako.
Hosana juu, hosanna juu,
Hosana juu, hosanna juu mbinguni *2
Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina.
Mbarikiwa yeye *2 ajaye kwa jina la Bwana.
Ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu, hosanna juu,
Hosana juu, hosanna juu mbinguni *2
Mystery Of Faith
Yesu Kristu alikufa *2, Yesu Kristu alifufuka
Yesu Kristu atakuja tena.
Gospel Acclamation
Alleluia! *n
Great Amen
Amina ah *n