Back to repertoire
Swahili

Bwana Ni Mchunga

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

1. Bwana ni Mchunga, sitahitaji
Majani mabichi, malisho yangu
Ananinywesha maji matulivu
Atanirudisha nikipotea
2. Nipitapo bondeni mwa mauti,
U mlinzi wangu, sitaogopa
Fimbo lako latosha kunilinda,
Ukinifariji sina hasara
3. Kati ya mateso meza waandaa
Na kikombe changu kinafurika
Umenipaka kichwani mafuta,
Nitaulizaje zaidi kwako
4. Wema na Fadhili vinifuate
Siku zangu zote hata milele
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika ufalme wa pendo lake

Liturgical seasons

Mass parts

Communion