Back to repertoire
Swahili

Bwana Hebu Tuokoe

Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.

Lyrics

1. Bwana hebu tuokoe! Mawimbi ni makubwa!
Kuna giza kwenye mawingu, hakuna msaidizi;
Hujali twaangamia? Mbona unalala,
Wakati mawimbi yanatisha, kuyaleta mauti?

Mawimbi na upepo vilitii, Amani!
Bahari ikasirike, mapepo hata watu na vitu vyote
Meli yangu haiwezi kuzama Bwana akiwa ndani yangu.
Vitu vyote vitamtii, tuwe na amani.
Vitu vyote vitatii tuwe na Amani.

2. Bwana niko na huzuni, katika siku hii,
Roho yangu inasumbuka Njoo uniokoe;
Kuna mawimbi ya dhambi yaliyo moyoni,
Bwana mimi ninaangamia Hebu nisaidie.
3. Sasa hakuna matata, kuna mapumziko,
Sasa jua laonekana, mbingu iko karibu,
Usichelewe Ee Bwana, na usituwache,
Kwa furaha nitaweka nanga kwenye ufuo wako.

Liturgical seasons

Mass parts

Communion