Bwana Anakuja
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Bwana anakuja, twendeni kumlaki, Bwana Mungu wa majeshi.
Ziwasheni nyoyo tukamkaribishe, Huyu mwenye utukufu
Karibu Bwana, Njoo (x2),
Shinda pamoja nasi
1. Wewe ndiwe Mkate, Mkate wa mbinguni, Utulishe wenye njaa.
Wewe ndiwe Mwanga, sisi tu vipofu, tufanye tuone tena.
2. Wewe ndiwe Njia, tutakufuata, tumrudie Baba Yetu.
Wewe ni Ukweli, utuangazie, tusije tukapotoka
3. Wewe ni Uzima, sis tu wagonjwa, twakujia utuponye.
Tumwendee nani tukilemewa? Kitulizo chetu Wewe
4. Wewe ni Mzabibu, sisi tu matawi; tuungane siku zote.
We’mchungaji mwema, tunakutambua, tuongoze malishoni
5. Hosanna hosanna Huyu mmbarikiwa anakuja kwetu sisi
Ajakutulisha na kutugawia matunda ya ukombozi
6. Bado tu njiani; yadumu imani, tumaini na upendo.
Saa ya kufa kwetu tupate kuona Uso wako wa rehema, tusije tukapotoka