Back to repertoire
Swahili
Amepaa
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Amepaa amepaa juu Mbinguni *2
1. Nimepewa mamlaka yote, aleluya
Mbinguni na duniani, aleluya
2. Nendeni mkawafanye mataifa yote, aleluya
Wawe wafuasi, aleluya
3. Wabatizeni kwa jina la Baba na mwana aleluya
Na la Roho Mtakatifu aleluya
4. Wafundisheni kushika maagizo yote, aleluya
Niliyowapeni, aleluya
5. Nami nipo nanyi siku zote, aleluya,
Naam, mpaka mwisho wa nyakati, aleluya.
6. Nilitoka kwa Bwana, aleluya,
Nimefika duniani, aleluya
7. Ninaacha tena dunia, aleluya,
Niende kwa Baba, aleluya.
8. Kristu Bwana amepaa kwenda kwa Baba, aleluya,
Astahili sifa na heshima, aleluya.
Liturgical seasons
Mass parts
Communion