Back to repertoire
Swahili
Alfajiri ya Kupendeza
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
T: Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema siku yenye baraka
W: Jua limekwisha chomoza laamsha wote waliolala
Ndege nao wanalialia kumshukuru Muumba (Njooni)
{Njooni baba mama na watoto njoni wote mbele za Bwana
Tumtolee shukrani zetu, kwa kutoa sadaka *2)
1. Ndege wanamshukuru, kwa sauti za kupendeza
Na sisi tumshukuru, kwa zawadi alizotupa (njooni)
2. Wanyama pia na mimea, vyote vimeumbwa na Mungu
Vitu vyote vya duniani, vyapaswa kumshukuru Mungu (njooni)
3. Aliumba dunia hii, kaweka giza pia mwanga
Mchana tufanyeni kazi, usiku na tupumzike (njooni)
Liturgical seasons
Mass parts
Entrance