Back to repertoire
Swahili
Aleluya Tumwabudu Yesu Kristu
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
1. Aleluya tumwabudu Yesu Kristu
Yu hai mzima katika ekaristi
Aleluya aleluya aleluya
2. Sakramenti kuu hii ya mapendo,
Ulimojiweka kwa ajili ya watu,
Nasi twakupa yetu leo mapendo.
3. Ni sadaka ya msalaba twaijua,
Kafufuka kisha kapaa kwa Baba,
Yuko nasi katika hii Ekaristi.
4. Ni chakula chetu bora na kwa roho,
Ni Mwanakondoo yule wa pasaka,
Atulisha, atushibisha daima.
5. Njoni wote tumwabudu Yesu Kristu,
Nyoyo zetu, nyimbo zetu tumtolee,
Sifa zetu, shangwe zetu tumpatie.
6. Mwili wako uwe asili ya heri,
Utakase nyoyo zetu kwa damuyo,
Zifike mbinguni daima milele.
Liturgical seasons
Mass parts
Thanksgiving