A.M.E.C.E.A. Mass
Also known as: Amecea Mass · Misa Amecea · Amecea · A.M.E.C.E.A. · Sanctus – Amecea Mass
Copyright status has not been confirmed, so files are restricted to choir members.
Lyrics
Kyrie
Bwana utuhurumie (ee Bwana) - Bwana utuhurumie x2
Kristu utuhurumie (ee Kristu) - Kristu utuhurumie x2
Bwana utuhurumie (ee Bwana) - Bwana utuhurumie x2
Gloria
1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na Amani kote duniani
(Kwa watu) wenye mapenzi mema
Tunakusifu Baba tunakuheshimu, twakuabudu sisi tunakutukuza *2
2. Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu - wako mkuu ewe Mungu Mfalme
(Ee Baba) wa mbingu Baba yetu.
3. Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu - Mwana wa pekee wake Mungu
(Uliye) - Mwanakondoo wa Mungu.
4. Unayeziondoa dhambi zote - za dunia utuhurumie
(pokea) pokea ombi letu.
5. Wewe unayeketi kuume - kwake Baba utuhurumie
(sikia) - sikia ombi letu.
6. Kwani pekee yako ndiwe Bwana - Pekee yako mkuu na Mkombozi
(Pekee) - pekee Yesu Kristu.
7. Kwa umoja wa Roho Mtakatifu - ndani yake Baba watukuzwa
(Ee Yesu) - milele na milele.
Sanctus
Mtakatifu Mtakatifu Bwana, Mungu wa majeshi *2
Mbingu na dunia zimejaa zimejaa
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako x2
Hosana juu x 4 Mbinguni
Mbarikiwa ‘nayekuja *2 Mbarikiwa
Mbarikiwa ‘nayekuja kwa jina jina lake Bwana
Hosana juu x 4 Mbinguni
Mystery Of Faith
Yesu Kristu alikufax, Yesu Kristu kafufuka
Kristu atakuja atakuja kwetu tena (Yesu).
Great Amen
Amina *n
Aleluiyah *6
Agnus Dei
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi, za dunia (ee Mwana) utuhurumie x2
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi, za dunia (ee Mwana) utujalie amani
Gospel Acclamation
Alleluia *6